![](http://eatv.tv/sites/default/files/styles/detailpageimg/public/news/2024/03/22/kodi.jpg?itok=nGZRgjIz×tamp=1711123272)
Afisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mwenye fulana rangi ya njano akimsikiliza mfanyabiashara
Zoezi hilo linaenda sambamba na ukusanyaji wa maoni na changamoto na malalamiko kutoka kwa wafanyabiashara hao kwa lengo kwenda kuyafanyia kazi kwa lengo la kuboresha zaidi na hatimae kurahisisha ulipaji kodi kwa hiyari.
Miongoni mwa changamoto zilizoripotiwa ni pamoja na umbali wa upatikani wa huduma, ambapo wafanyabiashara wanapotaka huduma za TRA wanalazimika kusafiri kwa masafa marefu kufuata huduma hiyo jambo linalowangezea gharama wanazotumia katika usifiri na muda mwingi
Aidha, baadhi ya wafanyabiashara wamefurahishwa na zoezi hilo ambalo limewasaidia kufamahu mambo mbali mbali ya kodi na kushauri zoezi hilo liwe endelevu ili waendelee kujifunza zaidi.