Wednesday , 28th Feb , 2024

Staa mwimbaji wa muziki wa Afrobeat kutoka Nigeria Ayra Starr (21) amefanya mahojiano na Billboard na kufunguka kuwa alihitimu chuo akiwa na umri mdogo sana, miaka 17 tayari alikuwa na degree.

 

Mkali huyo wa Mavin Records amefunguka kuwa mama yake alikuwa akimzuia kukimbilia kwenye muziki kabla hajahitimu masomo, kwasababu aligundua Ayra alikuwa akiutamani umaarufu katika umri mdogo. Hivyo Ayra alianza chuo akiwa na umri mdogo (miaka 14) na baada ya chuo akajitupa moja kwa moja kwenye muziki.

Ayra Starr ambaye ni mzaliwa wa Benin na baadaye kuhamia Lagos, Nigeria, amehitimu Shahada ya Uhusiano wa Kimataifa na Masuala ya Siasa katika Chuo cha Les Cours Sonou kilichopo Cotonou Benin aliposoma kwa miaka mitatu.