Rais Dkt. Mwinyi akizungumza na Wafanyabiashara wa Soko Kuu la Jumbi leo Februari 26, 2024 wakati wa ziara yake ya kusikiliza changamoto zao
Rais Dkt. Mwinyi amesema hayo akizungumza na Wafanyabiashara wa Soko Kuu la Jumbi na Soko la samaki Malindi Mkoa wa Mjini Magharibi Februari 26, 2024 katika ziara yake maalumu ya alipotembelea masoko na kusikiliza changamoto zao.
Aidha, Dkt. Mwinyi amewaomba wafanyabiashara kutopandisha bei ya vyakula kiholela bila ya sababu za msingi kwa kupandisha mara mbili ya bei ili kuwasaidia wananchi wanyonge kuelekea Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.