Monday , 5th Feb , 2024

Wananchi wa kijiji cha Ikombe kata ya Matema Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya wamemkabidhi  Meneja wa shirika la Umeme nchini TANESCO Wilaya ya Kyela Kibatali ikiwa ni ishara ya kuachana na matumizi ya mafuta ya taa na umeme wa wa jua kwa matumizi mbalimbali. 

Hayo yamejiri baada ya wananchi hao kufikiwa na nishati ya umeme wa gridi ya taifa kwa mara ya kwanza kupitia Mradi Usambazaji  Umeme Vijijini REA.

"Ulivyofika umeme matarajio yetu kutakuwa na biasahara nyingi katika kijiji chetu cha Ikombe maana umeme ndo kila kitu kwa ajili biashara watu watakuwa na saloon" - Imani Makolo, Mkazi wa Ikombe

"Ambacho tutafaidika hapa ikom be baada ya kufikiwa na umeme watoto wataweza kujisomea hata usiku kwani walikuwa wanashindwa kujisomea usiku  kufuatana na mwanga tulikuwa hatuna na ndao kitu ambacho tumefurahi  sisi wanakijiji cha ikombe na tunaamini watoto wanasoma vizuri" - Esteria Hanji, Mkazi wa Ikombe

"Tuliakuwa tunatumia vibatari au mishumaa na sola kwa hiyo upande wawafunzi ilikuwa changamoto sana kujisomea ilikuwa mpaka mtu akanunulie mishumaa  au mafuta ya taa awashe koroboi  hali hiyo kunakuwa hakuna tena mwanafaunzi kujiosomea" - Felista Kimbiu, Mwananchi Kijiji cha Ikombe

"Watumishi wenzangu wanafuraha  ni siku nyetu kwetu ni siku tumekuwa tunatumia mwanga wa sola ambao si wa uhakikka kwani mmvua ikinyesha muda mrefu kuna kuwa hakuna tena mwanga hivyo kutuletea tabu hasa wakti wa mama kujifungua nyakati za usiku hivyo basi ujio wa umeme tumepata mwarobaini wa tatizo letu" Joshua Katabazi, Mganga Mfawidhi Zahanati ya Ikombe

Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya  Josephine Manase  amewataka wananchi  kutunza miundombinu  lakini  kutumia nishati ya umeme kujieletea maendeleo huku Meneja wa mradi  Mustapha Himba akieleza gharamza za mradi.

 "Umeme huu uende ukatukomboe ukatusaidie kiuchumi lakini utakwenda kubadilisha taswila ya kijiji chetu cha Ikombe kwa hiyo niwaome tuchangamkie hii fursa lakini pia ulinzi wa mindombinu kwani serikali imetumia gharama kubwea kufikasha umeme katika katika kijiji cha Ikombe" - Josephine  Manase, Mkuu Wa Wilaya Kyela

"Katika utelezaji wa mradi kyela tulikuwa na vijiji thelathini na tano na mpaka sasa tumeshawasha vijiji thelathini na tano kwa na hiki tulicho washa laeo niche thelathini na nne hivyo bado kijiji kimoja" Mustapha Himba, Meneja wa mradi REA.