Friday , 2nd Feb , 2024

Huwenda kila mtu anajua kupika, ila linapokuja suala la kiwango gani na unampikia nani? ndipo tui na machicha yanapojitenga.

 

Tanzania ilifurahi pale EastAfricaRadio ilipokuja na kampeni ya #MamaLishe ilipochukua jukumu la kuthamini kile wanachokifanya, zilikuwa ni wiki za mafuta kuchemka, jasho kutiririka na nafsi kujawa na woga kwani ilitakiwa wapatikane wachache kati ya wengi waliyojitokeza.

Tukasimama kwenye #KijasiriZaidi tukaonyesha ni namna gani #TogetherTunawakilisha wadau na wahafidhina wafia mapishi walikuwa nasi kwenye kuwapongeza na kuwatia moyo #MamaLishe 

Tumaini jipya likazaliwa kwa #MamaLishe waliopata wasaa wa kurudi darasani, ishukuriwe @kitm_dsm mapishi yalisomwa kwa kiwango cha juu. utofauti na mabadiliko kwenye mapishi ukaonekana ndani yao.

Rasmi leo wamehitimu na kuhesabiwa rasmi kama wataalamu kwenye suala la mapishi, Msimu wa nne siyo ukomo kwenye #MamaLishe kwani #MamaMia iko kumshika mkono kila mwanamke anayeonyesha juhudi kwenye jamii yake.