Friday , 2nd Feb , 2024

Shirika la Kiserikali la China linalosimamia utangazaji wa utalii  na uwekezaji  (China Tourism Group - CTG) limeonesha nia ya kutaka kutangaza vivutio vya utalii vilivyoko nchini Tanzania pamoja na kuwekeza katika maeneo mbalimbali ya sekta ya utalii nchini kwa lengo la kukuza utalii wa

Waziri wa Maliasili na Utalii, Angellah Kairuki

wa Tanzania na kuongeza mapato yatokanayo na sekta hiyo.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Angellah Kairuki katika kikao kati ya shirika hilo pamoja na Watendaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii kilichofanyika Jijini Dodoma.

Akizungumza katika kikao hicho, Waziri Kairuki amesema  Tanzania itanufaika na ushirikiano huo ambapo moja ya kipaumbele cha Serikali kwa sasa ni kuvutia watalii wengi kutoka nchi za nje hivyo, Serikali itatumia fursa hiyo kuvutia watalii kutoka soko la China.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa China Tourism Group, Dkt. Luo YANQING amesema lengo la ziara yake nchini Tanzania ni kufanya tafiti ya kuangalia maeneo ya uwekezaji wa hoteli pamoja na kuangalia namna ya  kuleta kundi kubwa la watalii wa Kichina nchini, ili watembelee vivutio na kuitangaza Tanzania kwa kuwa China kila mwaka takribani watalii milioni 170 wanatoka nje ya nchi  kutalii ikiwa ni takwimu za  mwaka 2019.