Na kumbuka mchezo mmoja Kazan tulipoenda kwenye michuano ya UEFA, kwenye mchezo ule washambuliaji wangu wote walikuwa majeruhi, hakuwepo Milito hakuwepo Eto'o nilikuwa kwenye kipindi kigumu sana na Balotelli ndiye aliyesalia pekee
Kwenye dakika kati ya 42 au 43 Balotelli alikuwa amekwisha pewa kadi ya njano kwenye ule mchezo, Tulipoenda kwenye chumba cha kubadili nguo muda wa mapumziko, Nilitumia dakika 14 kati ya 15 kuongea na Balotelli
Mario siwezi kukubadilisha na siwezi kufanya mabadiliko, sina mshambuliaji yeyote kwenye benchi, usimguse mtu yoyote wewe cheza na mpira pekee, ikiwa kama mwamuzi kafanya makosa basi usifanye chochote Mario nakuomba.
Dakika ya 46 baada ya kuanza kwa kipindi cha pili, Balotelli kapewa kadi nyekundu''
Chanzo: sbf_pod