Thursday , 18th Jan , 2024

Mamlaka nchini Msumbiji zina wasiwasi kuhusu ugonjwa wa ajabu ambao umeua zaidi ya ng'ombe 900 katika eneo la kati la nchi hiyo tangu mwezi Disemba mwaka jana.

Ugonjwa huu haujulikani kwa wafugaji na mamlaka za mifugo. Ililipuka katika mkoa wa Manica, kwenye mpaka na Zimbabwe na imeenea katika wilaya tatu za mkoa huo.

Wafugaji wenye wasiwasi wanaomba majibu ya haraka kutoka kwa mamlaka za mifugo ili kuzuia hasara zaidi, huku kukiwa na hofu kwamba ugonjwa huo unaweza kuenea na kuua ng'ombe zaidi.

Fernando Cupenha, mfugaji kutoka kijiji cha Manhene, katika wilaya ya Manica, moja ya mikoa iliyoathiriwa zaidi na mlipuko huo, alisema kuwa ugonjwa huo unahusishwa zaidi na kupoteza hamu ya kula na nguvu kwa wanyama.

Anaonya kuwa ugonjwa huo unaweza kuhatarisha usalama wa chakula na maisha.Luís Sabonete, mkulima mwingine, amelalamika kuwa mamlaka ya mifugo ya mkoa haijajibu tangu walipochukua sampuli za damu kutoka kwa wanyama wagonjwa kwa uchambuzi.

Mapema mwaka jana, ugonjwa wa nadra uliosababishwa na mbu uliua karibu vichw ng'ombe 400, katika kijiji cha Chinhambudzi, mkoa wa mpakani na Zimbabwe, pia katika mkoa wa Manica.