Friday , 12th Jan , 2024

Wanafunzi zaidi ya 1000 wa darasa la nne wamefeli mtihani wa Taifa wilayani Nyangh’wale mkoani Geita jambo ambalo limepelekea wilaya hiyo kufanya kikao cha tathimini na mipango ya elimu kwa mwaka 2024.

Akizungumza katika kikao hicho mkuu wa wilaya ya Nyangh’wale Grace Kingalame ameapa kuwawajibisha walimu na watendaji wa idara ya elimu wanaoshindwa kutimiza majukumu yao kwa mujibu wa sheria.

“Kwa yeyote ambaye ataki kutimiza wajibu wake anafanya business as usual kisa mshahara unaingia huyo nitadeal naye vizuri sana na wilaya ya Nyangh’wale itakuwa mfano Rais wetu dokta Samia analeta fedha kwaajili ya kujenga madarasa ameleta elimu bure watoto wetu wasome bila malipo arafu atokee mtu ataki kutimiza wajibu wake anaona kalumwa ni mbali sana kuliko dare s salaam hakuna atakaye mwona walimu huyo  nitadeal naye vizuri sana” amesema Grace Kingalame ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Nyangh’wale

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Nyangh’wale Husna Tonny amesema matokeo mabovu katika shule nyingi wilayani humo yanachangiwa na utoro unaosababishwa na watoto kukosa huduma ya chakula shuleni. 
“Kuna changamoto kubwa sana ya utoro kwa watoto wetu tumeona tuitane hapa tuchadili hili utoro unazidi

kuongezeka licha ya shule zetu kuwa na mazingira mazuri madarasa mazuri lakini bado utoro ni mkubwa na chanzo cha utoro ni kukosa chakula shuleni sasa hapo tujiulize tunashindwa nini wazazi kuwawezesha watoto wetu chakula wakala kwa utaratibu mzuri tutakao uweka tunapaswa tujali watoto wetu wapate lishe bora shuleni” Husna Tonny - Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Nyangh’wale

“Mimi ni msimamizi lakini pia ni mzazi kama hatujaweka mazingira mazuri kwa watoto wetu ambao watakuja kutusaidia baadae tutakuja kupata shida kubwa sisi kama wazazi tunapaswa kuwajali watoto wetu” Laurent Greison – Afisa Elimu wa Kata ya Nyabulanda

Nao baadhi ya walimu wa kuu wa shule waliouzulia kikao hicho wamesema wanaenda kuyafanyia kazi maagizo waliyopewa.

“Kutokana na matokeo ya darasa la nne kutokuwa vizuri kwa mikakati tuliyojiwekea leo ni wazi kwamba kwa mwaka huu 2024 tumejipanga vilivyo kuanzia walimu na wadau wa elimu wote kuakikisha shule zetu zinafanya vizuri”JALOS NYAMBALO-Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Ntetemia

“Tumebaini kwamba uwepo wa chakula cha mchana shuleni utasaidia kupunguza utoro kwa watoto nah ii itaongeza ufanisi kwa watoto na wataanza kufanya vizuri katika mitihani yao lakini pia watakao maliza darasa la saba wataongezeka tofauti na sasa ambapo wanaomaliza la saba ni wachache” - Deograsiana Mwangalaba - Mkuu wa shule ya sekondari Izunya