
Katika makubaliano hayo yaliyofikiwa kati ya vilabu hivyo viwili ni kuwa hakuna kipengele cha chaguo la kumnunua mchezaji huyo mara baada ya mkopo wake kumalizika.
Kwa muda mrefu sasa Sancho alikuwa akitaka kurejea Borussia Dortmund na amekuwa akifanya bidii kwa siku nyingi kufanikisha dili hilo na hatimaye limekamilika.