
Mwili wa mwanamke huyo ukiwekwa kwenye gari la polisi
Mwili wa mwanamke huyo umeonekana hii leo Januari 7, 2024, na taarifa za awali zimeeleza kuwa alifika hotelini hapo na mwanaume ambaye jina lake halijafahamika na kuchukua chumba na asubuhi ilipofika muda wa usafi waligonga bila mafanikio na mlango ulikuwa umefungwa na walipochukua fungua za ziada walikuta mwili uvunguni huku mwanaume huyo akitokomea kusikojulikana.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa mtaa amekiri kutokea kwa tukio hilo na kutoa wito kwa wanaume kutofikia hatua kama hizo kwani na kudai kuwa inaonekana mwanamke huyo ameuawa na mwanaume aliyefika naye katika eneo hilo.
Maafisa wa Polisi waliofika eneo la tukio na kuuchukua mwili wamesema kwamba taarifa zaidi zitatolewa uchunguzi utakapokamilika.