
Waziri Mavunde na watoto waliofiwa na mama yao
Hayo yamebainika baada ya kuwatembelea na kuwapa pole wananchi wa Kata ya Mbabala ambao walipata athari ya mvua kubwa iliombatana na upepo mkali ambapo pia ametoa msaada kwa waathirika wa tani 2 za mahindi, magodoro 50, sukari, maharage kilo 200 na maji katoni 100.
Akitoa taarifa ya athari hizo Mtendaji wa Mtaa wa Nguji, Mbabala Jumanne Misanga Njiku alieleza kuwa mnano mwezi Novemba mwishoni na Desemba 5, 2023, mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali ilileta athari kubwa kwa wakazi wa mitaa mitatu ya Kata ya Mbabala na kuwasabishia hasara kubwa ya mali ikiwemo upotevu wa mifugo na kupelekea kifo cha mama aliyekuwa amelala pamoja na watoto wawili ambao walidondokewa na nyumba na hivyo Bi. Rahel Nguselo kupoteza maisha na kuwaacha watoto wawili wadogo.
Akiwa hapo Mbunge Mavunde ametoa pole kwa wananchi wote waathirika kwa kadhia hii kubwa na kuwataka wananchi kuchukua tahadhari kubwa kwa mvua kubwa zinazoendelea kunyesha hivi sasa kama ambavyo imetabiriwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.
Aidha,Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Dodoma Charles Mamba, ametoa pole kwa waathirika wa majanga haya ya mvua na kuendelea kusisitiza juu ya kuchukua tahadhari kwa mvua kubwa zinazoendelea kunyesha hivi sasa katika maeneo mbalimbali ya Nchi.