
Aidha Waziri Bashe ameeleza kuwa Miundombinu ya kuhifadhia chakula nchini bado haipo vizuri kwa kiasi kikubwa ambapo kama serikali wanashirikiana na sekta binafsi ambao watasaidia kujenga maghala ya kuhifadhia chakula ili Kupunguza kiwango cha watu waonakwenda kuhifadhi mazao yao nje
Waziri Bashe ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam kwenye mkutano wa Kilimo uliowakutanisha viongozi wa serikali kupitia wizara ya Kilimo na wawezekaji wa ndani kwenye sekta ya Kilimo ili kujadili maendeleo ya sekta ya kilimo na kutathmini namna ya kukifanya kilimo kiwe na tija katika Biashara na pato la Taifa
Katika hatua nyingine waziri Bashe amesema wizara hiyo sasa imebadili mwelekeo na sasa wamejikita zaidi katika uzalishaji wa kujilisha wenyewe na kulisha wengine
"Tumebadili mwelekeo wetu kama sekta ya kilimo kwasasa tunajikita zaidi kwenye uzalishaji wa kujilisha wenyewe na kuwalisha wengine kiuchumi ili kupata pesa ambapo malengo ya sekta ya kilimo kwasasa ni kuongeza uzalishaji, kuongeza kiwango cha ushiriki wa vijana na wanawake kwenye kilimo, kuongeza usalama wa chakula, kuongeza soko la kilimo na kuweka mazingira shirikishi ya watu na wawezekaji kushiriki kwenye kilimo"