Thursday , 14th Dec , 2023

Rais Samia amemteua Maryam Muhaji kuwa Katibu Tawala wa mkoa wa Manyara ambapo kabla ya uteuzi huo alikuwa ni Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya ya Wanging’ombe na amechukua nafasi ya Karoline Albert Mthapula ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Rais Samia

Taarifa hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Zuhura Yunus, ambapo pia Rais Samia amemhamisha Zahara Michuzi kutoka Halmashauri ya Mji wa Geita kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara

Aidha Rais wa Tanzania, Dtk. Samia Suluhu Hassan amemteua Michael Kachoma kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega akichukua nafasi nafasi ya Veronica Vicent Sayore ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Hii hapa orodha ya walioteuliwa, kutenguliwa na kuhamishwa.