
jeneza lililobeba mwili wa Emmanuel Roman
Emmanuel ambaye imeelezwa amekuwa akisumbuliwa na afya ya akili alikutwa amefariki nyumbani kwake jana asubuhi Desemba 10 ambapo kwa mujibu wa mashuhuda akiwemo Mwenyekiti wa Kitongoji hicho James Malyos wamesema walimkuta Emmanuel akiwa kwenye kochi huku mkono wa kushoto ukiwa na grinder lililosadikika kuwa alitumia kujikata huku kukiwa na jeraha Shingoni.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Singida ACP Stella Mutabihirwa, akizungumza kwa njia ya simu amethibitisha kutokea tukio hilo na kusema bado wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo kabla ya kutoa taarifa kamili ili kubaini hasa kiini cha tukio hilo.