Friday , 24th Nov , 2023

Daktari wa klabu ya Yanga Moses Etutu amesema wachezaji wote wa kikosi cha timu ya Wananchi wapo salama kiafya na wapo tayari kwa ajili yamchezo wa kwanza wa klabu bingwa Afrika dhidi ya CR Belouizdad unaochezwa leo majira ya Saa 4:00 usiku kwa saa za hapa nyumbani Tanzania.

Yanga watashuka dimbani usiku wa leo ukiwa ni mchezo wao wa kwanza wa klabu bingwa hatua ya makundi tangu mwaka 1998 na mchezo huu ni wa kundi D. 
“Kwa ujumla afya za wachezaji wote ni salama, wako salama kabisa tulipata tu shinda kidogo wakati tunafika za homa na mafua wakati tunafika kutokana na hali ya hewa ya huku ya baridi lakini kwa sasa kila mchezaji yuko salama, wako very positive kwa ajili ya mchezo.” amesema Dakktari wa klabu ya Yanga Moses Etutu 

Wachezaji wote wa kikosi cha Yanga wameonekana wakiwa wapo na kikosi hicho kwenye mazoezi ya mwisho yaliyofanyika jana usiku, ikiwemo Golikipa Djgui Diara na kiungo Stephan Aziz Ki ambao walitwajwa huwenda wangeukosa mchezo huu. Kiungo wa kimataifa wa Uganda Khalid Aucho naye tayari amejiunga na kambi.