Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) Dkt. Said Mohamed
Hayo yamebainishwa leo Novemba 23, 2023, wakati Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), Dkt. Said Mohamed, akitangaza matokeo hayo, ambapo amesema masomo manne kati ya sita yaliyotahiniwa mwaka huu ufaulu wake umepanda.
"Takwimu zinaonesha kuwa Ufaulu wa somo la hisabati umeshuka kwa asilimia 4.46 na kufikia 48.83 ikilinganishwa na mwaka jana, katika somo la hisabati asilimia 51 ya watahiniwa wote wamepata daraja D, hata hivyo katika somo hili idadi ya watahiniwa walioopata grade A imeongezeka kwa silimia 0.33," amesema Katibu Mtendaji wa NECTA
Aidha akizungumzia watahiniwa waliofutiwa matokeo amesema, "Baraza limefuta matokeo ya watahiniwa 31 sawa na asilimia 0.002 ya watahiniwa wote waliofanya mtihani mwaka huu baada ya kubainika kufanya udanganyifu," - Dkt. Said Mohamed, Katibu Mtendaji NECTA