Thursday , 16th Nov , 2023

Msanii mkongwe Tanzania Mr II Sugu amesema hata yeye hajasoma sana elimu ya darasani lakini ametoboa kiaina kwenye maisha.

Picha ya Mr II Sugu

Sugu amefunguka hilo baada ya kupost picha ya msosi wa samaki, ndizi na salad kisha kuandika "Mlipokuwa mnaambiwa msome Elimu ni ufunguo wa maisha mkaleta ubishi sasa mnabaki mnatamani tu".

Mashabiki wengi wamemjia juu suala hilo la msosi na elimu wakimuhoji kwamba vinaingiliana vipi katika maisha ambapo amewajibu hata yeye hajasoma elimu ya darasani lakini ametoboa.

"Haya isiwe tabu bandugu, Mie mwenyewe sijasoma Elimu ya darasani kiivyo na nimetoboa kiaina" ameandika Sugu kwenye post yake mpya.