Tuesday , 14th Nov , 2023

Turudi nyuma mpaka miaka 15 iliyopita pale ambapo muziki ulipo wakutanisha Jordin Sparks na Christopher Brown na kutengeneza ''duet'' kali kuwahi kusikilizwa kwenye ulimwengu wa muziki'.

 

Ngoma iliyofanikiwa kushika nafasi ya tatu kwenye ''US Billboard Hot 100'' na namba moja kwenye nchi mbali mbali, kukutana kwa Jordin na Chris  ni matokeo ya BET award ya mwaka 2007 walipo kutana na kupanga kufanya ngoma hiii.

Kilichozungumzwa kwa ujumla ni kuhusiana na mahusiano ambayo kwa sasa hayapo tena. (watu waliotengena), maumivu unayohisi pindi unapokuwa mbali na mtu huyo, kiasi cha kuhisi huwezi kufanya kitu bila uwepo wake.

Kwenye moja ya mahojiano Jordin anasema kilichoimbwa kwenye ngoma hii kimetokana na uhalisia wake wa hali ya mahusiano baada ya kutengena na aliyempenda, lakini anasema kila kilichoimbwa kinaweza kuhusiana na mtu yeyote duniani anayepitia wakati mgumu baada ya kutengena na aliyempenda.

“Tell me how I’m supposed to breathe with no air / Can’t live, can’t breathe with no air / It’s how I feel whenever you ain’t there.”

Unatamani kurudisha nyuma wakati na kukumbikia kila mlichopitia pamoja, lakini unakumbuka muda hauwezi kurudi nyuma, hisia ambazo mtu anapitia baada ya kumpoteza anayempenda zimelinganishwa na uwezekano wa kuvuta pumzi bila uwepo wa oksijeni.

Tumekuuliza kwa upande wako, ni mtu gani ambaye huwezi kuishi bila uwepo wake? tuandikie hapo chini kwenye comment

Picha: blogspot.com|