Monday , 23rd Oct , 2023

Kocha msaidizi wa timu hiyo, Thabo Senong amesema licha ya kutambua ugumu wa mchezo huo ila kitendo cha kupata matokeo chanya kutoka kwa Namungo kimewaongezea morali wachezaji cha kuendelea kupambana zaidi.

“Kila mchezo ni mgumu lakini maandalizi bora siku zote ndiyo yanayoamua, kwetu ni changamoto nyingine iliyopo mbele yetu ambayo tunakabiliana nayo, tunaiheshimu Yanga ila hatutakuja kinyonge kwani tunahitaji kupata pointi tatu pia,” amesema.

Kwa upande wa beki wa timu hiyo, Carno Biemes alisema ushindani umekuwa ni mkali katika kila mchezo wa Ligi Kuu, hivyo wachezaji wanatambua mashabiki zao wanahitaji nini na jukumu wanalo-paswa kulifanya kwa ubora kwa ajili ya kupata matokeo mazuri.

Huu utakuwa ni mchezo wa tatu kwa Singida kukutana na Yanga katika Ligi Kuu Bara na haijawahi kushinda kwani licha tu ya kupoteza kwa mabao 4-1 Novemba 17, mwaka jana ila mchezo wa mwisho uliopigwa Uwanja wa Liti Mei 4, mwaka huu timu hiyo ilichapwa 2-0.