
Takwimu hizi ni hadi mwanzoni mwa Oktoba - zinazofunika kipindi tangu nchi hiyo ilipotangaza mlipuko wa dengue mwezi Agosti, kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO).
Wizara ya afya ya Chad kwa sasa inakabiliana na mlipuko huo huku kukiwa na wasiwasi wa ugonjwa huo kusambaa zaidi kwa sababu ya uwezo mdogo wa ufuatiliaji na usaidizi.
Wilaya ya afya ya Abéché, katika mkoa wa kusini mashariki wa Ouaddai, ndio kitovu cha mlipuko wa sasa.
Dengue huambukizwa na mbu na mara nyingi husababisha dalili kali kama za mafua, bila matibabu maalum. Utambuzi na usimamizi wa wakati ni muhimu.
Kesi katika jamii zinaweza kuripotiwa kwa sababu waganga mara nyingi huchanganya dalili zake na maambukizi mengine, na kufanya utambuzi wa mapema kuwa changamoto, haswa katika maeneo yenye vifaa vichache vya upimaji.
WHO inataja mlipuko huo kama hatari kubwa ya kitaifa kutokana na mazingira mazuri ya kuenea kwa mbu na mgogoro unaoendelea wa kibinadamu katika eneo linalohusisha utitiri wa wakimbizi kutoka Sudan.