Thursday , 19th Oct , 2023

Mwanamitindo na mfanyabiashara maarufu duniani Kim Kardashian amesema anahitaji kuwa kwenye mahusiano na mwanaume ambaye amemzidi umri kwa sababu anavutiwa nao.

Picha ya Kim Kardashian

Kim Kardashian mwenye watoto wanne na rapa Kanye West 'YE' amesema anataka mwanaume kuanzia miaka 40 na kuendelea.

"Nahitaji mtu aliyenizidi umri kidogo ambao utanifaa. Nahitaji umri kama kuanzia miaka 40".

Mahusiano ya mwisho ya Kim Kardashian alikuwa na mchekeshaji na muigizaji wa Marekani Pete Davidson ambaye ana miaka 29.