
Wakizungumza na EATV wahanga wa tukio hilo wamesema usiku wa kuamkia Jumatatu baadhi yao walilazimika kulala nje kutokana na nyumba zao kuharibiwa na upepo.
“Jana jioni lilijitokeza wingu baada ya muda mfupi ukaanza kuvuma upepo tukawa tumekimbilia ndani mi na kijana wangu mdogo mara ghafla tukasikia kitu kinaanguka nikasema nyumba inaanguka mwanangu mwanangu akaniambia tukimbilie wapi nikamwambia tutoke ndani twende nje kuja kuangalia tukaona nyumba nzima imejaa vumbi” - Ester Lukebela mkazi wa kata ya Shabaka
Diwani wa kata hiyo Kalimu Hamis Chasama akithibitisha kutokea kwa tukio hilo amesema upepo huo pia umesababisha maafa kwenye taasisi za serikali.
“Kwenye kata yangu ni nyumba nyingi ambazo zimeezuliwa na upepo kama mia moja na kitu kwa taarifa nilizopata mpaka sasa lakini pia kuna kwenye taasisi za serikali kama choo cha shule ya msingi Lubado kimeezuliwa,Darasa moja shule ya msingi muhama limeezuliwa lakini pia jengo moja la kununulia pamba katika kijiji cha muhama nalo limeezuliwa” - Kalim Hamis Chasama Diwani wa Kata ya Shabaka