Tuesday , 17th Oct , 2023

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken ametangaza kuwa Rais wa wa taifa hilo Joe Biden anatarajiwa kuzuru Israel siku ya Jumatano huku mzozo wa Gaza ukiongezeka

Tangazo hilo limetolewa katika ubalozi wa Marekani mjini Jerusalem baada ya mkutano wa saa saba kati ya mwanadiplomasia mkuu wa Marekani Antony Blinken na Waziri Mkuu Netanyahu siku ya Jumatatu.

Imeelezwa kuwa malengo ya ziara hiyo ni kupokea taarifa za kina juu ya malengo na mkakati wa vita vya Israeli na kusikia kutoka kwa Israeli jinsi itakavyoendesha operesheni zake kwa njia ambayo itapunguza majeruhi ya raia pamoja na kuruhusu msaada kuwafikia raia wa Palestina huko Gaza.
 

Wakati hayo yakijiri Rais wa Urusi Vladimir Putin amewasili nchini China leo Jumanne kukutana na rais mwenzake wa China Xi Jinping na kuhudhuria mkutano wa kilele .

Mkutano huo ulioandaliwa na China unalenga kujadili maendeleo yaliyofikiwa na China katika miradi ya miundombinu kimataifa.

Xi na Putin wanatarajiwa pia kujadili masuala mbalimbali ikiwemo mzozo unaoendelea Mashariki ya Kati.