Mbappe kwa sasa anawakilishwa na mama yake mzazi Fayza Lamari kwenye masuala mengi ya mikataba, ambapo hali hiyo inaweza kusababisha matatizo linapokuja suala la kufanya mazungumzo ya kuhamia Madrid.
Hii ni kwa sababu sheria mpya ya FIFA inaelekeza kuwa uhamisho na mikataba unaweza kujadiliwa na mawakala wenye leseni pekee na Lamari ambaye ni mama mzazi wa Mbappe hayupo kwenye orodha ya mawakala wanaotambuliwa na FIFA, hivyo hawezi kumwakilisha mchezaji yeyote kwa misingi rasmi.
Hivyo Mbappe atalazimika kumfuta kazi mama yake mzazi na kutafuta wakala mwingine ambaye anatambuliwa na FIFA endapo atahitaji kufanikisha uhamisho wake wa kuelekea Madrid.