Friday , 6th Oct , 2023

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amelipongeza Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa uwekezaji wa mradi wa ujenzi wa viwanja vya michezo na Ofisi katika eneo la Kigamboni Jijini Dar es Salaam.

Mhe. Ndumbaro ametoa pongezi hizo hivi karibuni alipofanya ziara katika mradi huo, ambapo amesema Shirikisho hilo limepiga hatua kubwa katika kuendeleza Mpira wa Miguu pamoja na uwekekezaji katika miundombinu ya michezo.

Ametoa wito kwa Mashirikisho, vilabu na wadau mbalimbali wa michezo waige mfano huo ili Sekta ya michezo iendelee kupiga hatua zaidi.

Katika ziara hiyo Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Ndg. Wallace Karia alimueleza Waziri Dkt. Damas Ndumbaro kuwa upo mradi mwingine kama huo Jijini Tanga na nia ya Shirikisho hilo ni kuhamisha Ofisi zake kutoka Karume kwenda Kigamboni na eneo la Karume libaki kuwa eneo la viwanja.