Thursday , 28th Sep , 2023

Mabingwa watetezi wa kombe la Carabao Cup Manchester United wamepangwa kucheza na Newcastle United kwenye hatua ya mzunguko wa 4 wa michuano hiyo inayotarajiwa kuchezwa mnamo Oktoba 30-2023.

United huu unakuwa mchezo wao wa 12 mfululizo wakipangwa kucheza kuanzia  nyumbani huku mchezo dhidi ya Newcastle United ni kumbukumbu ya fainali ya msimu uliopita ambapo United ilishinda kwa magoli 2-0 kwenye dimba la Wembley. Michezo mingine kwenye mzunguko wa 4,

Mansfield watacheza na Port Vale,Ipswich dhidi ya Fulham,Bournemouth watacheza na   Liverpool ilhali Chelsea watapambana na  Blackburn,West Ham dhidi  Arsenal,Everton watacheza na  Burnley huku  Exeter watacheza na  Middlesbrough.