Thursday , 28th Sep , 2023

Nyota wa kikapu Damian Lillard amejiunga na timu ya Milwaukee Bucks inayoshiriki ligi ya kikapu ya Marekani (NBA) kwa kandarasi ya miaka 3 akitokea timu ya Portland Trail Blazers aliyodumu nayo kwa miaka 11 tangu mwaka 2012.

Lillard mwenye miaka 33 aliandika kwenye mtandao wake wa X zamani ukijulikana kama Twitter anasubiri kwa hamu kusubiri msimu mpya wa NBA kwa ajili ya kuitumikia timu yake mpya ya Milwaukee Bucks.

Damian Lillard alitangazwa kuwa miongoni  mwa  wachezaji 75 bora kuwahi kucheza ligi ya kikapu ya NBA mnamo mwaka 2021 huku msimu uliopita alikuwa na wastani wa kufunga alama 32.2 kwa mchezo mmoja na sasa anaungana  na MVP mara mbili wa NBA Mgiriki Giannis Antetokounmpo ndani ya Bucks.