Wednesday , 25th Feb , 2015

Star wa muziki Matonya, ambaye kwa sasa anatikisa chati na ngoma yake inayokwenda kwa jina 'Homa ya Jiji', amesema baada ya kipindi cha kutingwa na mambo yaliyokuwa yanamuweka nje ya gemu, sasa amerejea kikazi zaidi.

Matonya

Wakati akirejea Matonya pia amekaribisha wale wanaotaka kufanya naye kazi kufanya hivyo sasa.

Matonya ambaye pia hivi karibuni ametangaza kuwa anatoa ngoma kila mwisho wa mwezi, amesema kuwa yupo kikazi zaidi sasa, majukumu yake binafsi yakiwa yamekaa sawa na kutoa nafasi kwa yeye kuirudia nafasi yake.