Monday , 25th Sep , 2023

Raia wa Kenya mwenye miaka 26 amekamatwa Jana Jumapili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bandaranaike (BIA) huko Katunayake, Sri Lanka wakati akijaribu kusafirisha kilo 4 za dawa za kulevya aina ya cocaine yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 136 za Kenya sawa na Tsh bilioni 2.3

Dawa zilizokamatwa

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Sri Lanka, vimeeleza kuwa mtu huyo pia ni mfanyabiashara wa magari na alikuwa amewasili nchini humo akitokea Ethiopia kupitia Qatar.

Madawa hayo yalinaswa na kitengo cha kudhibiti dawa za kulevya baada ya kubaini kete za madawa hayo zikiwa zimefichwa kwenye makopo ya biskuti.