Muungano wa Free Current ulisema kuwa Hisham Kassem amekuwa mgombea wa urais anayetarajiwa. Alipatikana na hatia ya kukashifu na kumshambulia kwa maneno afisa wa polisi.
Wafuasi wake wanasema mashtaka hayo yalichochewa kisiasa.Rais Abdul Fattah al-Sisi anatarajiwa kutangaza kuwa atawania muhula wa tatu, lakini bado hajafanya hivyo.
Mtu pekee ambaye ametangaza kugombea hadi sasa, Ahmed al-Tantawi, amesema timu yake imekabiliwa na unyanyasaji unaoongezeka na vikosi vya usalama.