Kikosi kimeondoka na benchi zima la ufundi likiongozwa na kocha Mkuu Roberto Oliviera ‘Robertinho’.
Baada ya kufika Zambia kikosi kitafanya mazoezi ya mwisho kesho jioni katika Uwanja wa Levy Mwanawasa ambao tutautumia kwa mchezo wetu wa Jumamosi.
Wameondoka nchini Tanzania wakiwa na matarajio kikabo ya kufanya vyema kwenye mchezo huo mgumu na wanaiheshimu Power Dynamos lakini wamejipanga kufanya vizuri.
Huku wakiingia kwenye mchezo wakiwa na lengo moja la kutafuta ushindi kwenye mchezo wa ugenini ili kujiweka kwenye mazingira mazuri katika mechi ya mkondo wa pili utaopigwa jijini Dar es salaam.