Tuesday , 12th Sep , 2023

Ripoti zinaonesha kuwa idadi ya Wakenya wanaotumia bangi kwa wingi imeongezeka jambo ambalo linaonesha kushangaza zaidi kwa kipindi cha miaka mitano ikihusisha kwa vijana zaidi.

Bangi

Utafiti mpya uliotolewa na Mamlaka ya Kupambana na Matumizi Mabaya ya Pombe na Madawa ya Kulevya nchini Kenya (NACADA) unaonesha kuwa matumizi ya mihadarati nchini humo yameibua wasiwasi na kwamba wanaotumia bangi na vileo wako kwenye hatari zaidi ya kupata sonona na msongo wa mawazo, ambao ni mara 2.3 zaidi ikilinganishwa na wasiotumia.

Takribani mtu mmoja kati ya 26 (watu 475,770) kwa sasa wanatumia bangi nchini humo, huku Jiji la Nairobi likiongoza kuwa na kiwango kikubwa cha watumiaji wa bangi.