Thursday , 7th Sep , 2023

Mexico inaonekana kuwa na uhakika wa kumchagua kiongozi wake wa kwanza mwanamke baada ya Claudia Sheinbaum kuthibitishwa kuwa mgombea wa chama tawala katika uchaguzi wa rais wa mwaka ujao.

Claudia Sheinbaum amethibitishwa kuwa mgombea wa chama tawala katika uchaguzi wa rais wa mwaka ujao

Meya huyo wa zamani wa Mexico City atakabiliana na Xóchitl Gálvez, ambaye anaongoza muungano wa upinzani.

Bi Sheinbaum, mwanasayansi mwenye umri wa miaka 61, ni mshirika wa karibu wa rais wa mrengo wa kushoto Andrés Manuel López Obrador. aliwaambia wafuasi wake katika hotuba yake kwamba

"Tutashinda mwaka 2024,"

Sheinbaum aliwashinda wagombea wengine watano na kushinda kila uchaguzi wa tano, ikiwa ni wastani wa asilimia 39 ya kura, chama cha Morena kilitangaza.

Akiwa kiongozi wa wanafunzi katika miaka ya 1980, Bi Sheinbaum alihudumu kama katibu wa mazingira wa Mexico City wakati Bwana López Obrador alipokuwa meya kutoka 2000 hadi 2005.

Baadaye alihudumu kama meya wa jiji la Mexico kuanzia mwaka 2018 hadi mapema mwaka huu alipojiuzulu kuwania urais.

Bi Sheinbaum aliliambia gazeti la Gatopardo kwamba "Wasichana wanaona mfano ndani yangu," "Kuwa rais wa kwanza mwanamke itakuwa ni jambo la kihistoria katika nchi yetu."