
Bw. Vianey ameyasema hayo leo Septemba 06, 2023 katika mahojiano na East Africa Radio wakati akielezea namna ambavyo Tanzania inaweza kunufaika na uwepo wa mkutano huo ambao unafanyika kwa takribani siku nne kuanzia Septemba 5-8 mwaka huu 2023.
Katika mahojiano hayo Bw. Vianey amesema ni lazima sasa kama nchi na wadau wa sekta ya kilimo wafikirie namna ya kuwavutia wawekezaji wengi ili kuongeze ushindani ambao utasaidia kushusha bei ya teknolojia.
"Lakini siyo bei tu kama upatikanaji wa pembejeo zikipatikana kwa wakati maana yake ni kwamba hata sisi tutaweza kulima kwa wakati na tutapata tija kubwa na kuongeza ushindani wetu kwenye soko la kimataifa" amesema Vianey Rweyendela, Meneja Mkazi kutoka AGRA
Aidha, Bw. Vianey amesema katika ripoti ya Mifumo ya Kilimo Africa ya kila mwaka imebainisha kuhusu umuhimu wa kutengeneza mifumo endelevu ya chakula kwa siku zijazo ambapo lazima nguvukazi iliyopo itumike kwaajili ya uzalishaji.
"Ili tuzalishe chakula katika mazingira endelevu lazima tuanze na populationi iliyo chini ili wakue na teknolojia ya uzalishaji, uzalishaji hauwezi kukua kama hatutumii teknolojia na hatuwezi kuwa na chakula cha kutosha kama teknolojia haitumiki"
"Idadi ya watu ikikua na chakula hakizalishwi kulingana na idadi ya watu uwezekano wa kutokuwa na chakula kwa siku zijazo ni mkubwa sana ndiyo maana tunasema tuwaingize vijana wanaoweza kuichukua teknolojia kwa urahisi kuliko watu wazima kwa sababu kilio bila teknolojia hakiwezi kuendelea" amesema Vianey Rweyendela
Sambamba na hayo bado matumizi ya teknolojia bado yanasisitizwa katika uzalishaji endelevu wa chakula ambapo Bw. Vianey amebainisha kuwa rasilimali vijana ambao wanaweza kuichukua teknolojia kwa urahisi zaidi inatumika kuliko watu wazima kwa sababu kilio bila teknolojia hakiwezi kuendelea.