Tuesday , 5th Sep , 2023

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un anapanga kusafiri kwenda Urusi mwezi huu kukutana na Rais Vladimir Putin, kwa mujibu wa taarifa ya afisa mmoja wa Marekani

Viongozi hao wawili watajadili uwezekano wa Korea Kaskazini kuipatia Moscow silaha za kusaidia vita vyake nchini Ukraine, afisa huyo alisema.Ambapo mazungumzo yatafanyika sehemu isiyojulikana.

Msemaji wa Kremlin hakuwa na cha kusema juu ya ripoti hizo, ambazo pia zilibebwa na vyombo vingine vya habari vya Marekani. Hakuna tamko lolote la haraka kutoka Korea Kaskazini.

Vyanzo vya habari vimeliambia gazeti la New York Times kwamba Kim alikuwa na uwezekano mkubwa wa kusafiri kwa kutumia treni ya kivita.

Mkutano huo unakuja baada ya Ikulu ya White House kusema ina taarifa mpya kwamba mazungumzo ya silaha kati ya nchi hizo mbili yanaendelea.

Msemaji wa Baraza la Usalama la Taifa John Kirby amesema Waziri wa Ulinzi wa Urusi, Sergei Shoigu, alijaribu kuishawishi Pyongyang kuuza silaha za kivita kwa Urusi wakati wa ziara yake ya hivi karibuni nchini Korea Kaskazini.