Friday , 1st Sep , 2023

Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya linamshikilia Bibi Malogi Lyobelo Mwaihoyo (75), mkazi wa Kijiji cha Ikoho Kata ya Maendeleo wilayani Mbalizi mwenye uoni hafifu kwa tuhuma za kumuua mjukuu wake Vision Erick (1) kwa kumkata na jembe kichwani wakati wakichimba udongo wa kukandikia nyumba yake.

Jembe

Akizungumza Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya ACP Benjamin Kuzaga amesema tukio hilo limetokea Agosti 30 mwaka huu wakati bibi huyo mwenye uoni hafifu akisafisha eneo na kuchimba udongo wa kwa ajili ya kukandikia nyumba yake.

"Mtoto Vision Erick alifariki baada ya kukatwa kwa jembe kichwani na bibi yake na chanzo cha tukio hilo ni kwamba huyu bibi mwenye miaka 75 ambaye ana uoni hafifu kama nilivyosema alikuwa anasafisha sehemu ya kuchimba udongo wa kukandikia nyumba," amesema Kamanda Kuzaga.