Friday , 1st Sep , 2023

Hassan Ngema mkazi wa kijiji cha Itegete wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro ameuawa kwa kile kinachodaiwa kushindwa kulipa deni la muda mrefu la mahari ya shilingi  laki tano.

mikono

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro ACP Alex Mkama, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kutokana na tukio hilo watu wanne wa familia moja wanashikiliwa kwa tuhuma za kufanya mauaji hayo akiwemo baba mkwe wa marehemu ambae ni bwana Masele Machibya ambae ni mkazi wa mkoa wa Tabora.

"Wengine tulioowakamata ni Machibya Masele kwa pamoja walikula njama na kumuua Hassan Ngema baada ya kushindwa kulipa mahari na upelelezi utakapo kamilika watafikishwa mahakamani," amesema ACP Mkama

Nae Katibu wa Baraza la Masheikh mkoani Morogoro Sheikh Nassoro Hamisi Koba, amefafanua kwa kina juu ya suala la ulipaji wa mahari kwa sheria ya dini ya kiislamu na kusema haina muda wa kuilipa na kwamba inapendeza zaidi ikilipwa kwa wakati kwani ni haki ya mwanamke.