
Aliwapiga risasi wateja watatu weusi, wanaume wawili na mwanamke mmoja ambao hawajatajwa majina.
Kulingana na afisa mkuu wa polisi wa Kaunti ya Jacksonville, mwanamume huyo ambaye alikuwa na umri wa miaka 20 hivi pasi na kutajwa jina alikuwa amevalia vazi la kujikinga alipoingia kwenye kituo kinachojulikana kama dola akiwa na bunduki mfano wa SMG na bastola.
"Upigaji risasi huu ulichochewa na ubaguzi wa rangi na aliwachukia watu Weusi," Afisa mkuu wa polisi wa Kaunti ya Jacksonville, T K Waters amewambia waandishi wa habari Jumamosi.
Waters amesema mamlaka inaamini kuwa mshambuliaji alitenda jambo hilo peke yake na kwamba kabla ya shambulio hilo, alikuwa ameandika "ilani kadhaa" kwa vyombo vya habari, wazazi wake na vyombo vya sheria vinavyoelezea itikadi yake ya kueneza ya chuki.
Amesema mshambuliaji huyo alionekana katika chuo cha historia ya watu Weusi cha Edward Waters, ambapo alivaa fulana yake na barakoa kabla ya kwenda katika tawi la dula kubwa la bidhaa za bei ya punguzo nchini Marekani la Dollar General.
Kumekuwa na mfululizo wa visa vya ufyatulianaji risasi nchini Marekani katika siku za hivi karibuni, na upatikanaji wa silaha kwa urahisi katika majimbo mengi na bunduki nyingi zaidi nchini kuliko raia.Mapema siku ya Jumamosi, takriban watu saba walipelekwa hospitalini baada ya ufyatulianaji wa risasi kwenye tamasha la Caribbean katika mji wa kaskazini mashariki wa Boston.
Usiku wa Ijumma wanawake wawili walipigwa risasi kwenye mchezo wa besiboli huko Chicago huku mtoto wa miaka 16 akipigwa risasi na kufa na wengine wanne kujeruhiwa baada ya ugomvi kwenye mchezo wa soka wa shule ya upili huko Oklahoma.