The Cask
"Jana jioni Mkurugenzi aliruhusu kuendelea na biashara zetu, tayari tumekamilisha kupata leseni ambayo ndiyo ilikua sababu ya kufungiwa," amesema Joel.
Patrick Masagati ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabiashara Tanzania mkoa wa Mwanza amesema jana jioni walikutana na mamlaka husika ndipo wakapewa majibu ya bar hiyo kuendelea na biashara zake kama kawaida.
Agosti 16, 2023, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ilemela Kiomoni Kibamba, aliifungia The Cask Bar kwa kwa siku 30 kwa alichoeleza kuwa haikuwa na leseni ya biashara kwa miaka miwili mfululizo.