Monday , 21st Aug , 2023

Kutokana na kuwepo na hali mbaya ya maambukizi ya ugonjwa wa Usubi katika wilaya ya Namtumbo iliyopo mkoani Ruvuma wilaya hiyo imejipanga kutokomeza ugonjwa huo baada ya wilaya hiyo kushika nafasi ya tatu kwa maambukizi kati ya wilaya 24 nchini ambazo bado hazijafanikiwa kutokomeza ugonjwa

Sababu potofu ya hofu ya kupoteza nguvu za kiume kwa wanaume ni sababu ya kushindwa kutumia dawa za Usubi.

Akiongea kwenye uzinduzi wa ugawaji wa dawa tiba ya Usubi ndugu Mansour Mgalula kutoka wizara ya afya kitengo maalumu cha kusimamia magonjwa ambayo hayapewi kipambele amesema wilaya nyingi nchini zimefanikiwa kutokomeza maambukizi ya ugonjwa wa Usubi lakini zimebakia wilaya 24 tu huku wilaya ya Namtumbo ikishika nafasi ya tatu katika maambukizi ya ugonjwa huo.

Wilaya nyingi zimefanikiwa kutokomeza ugonjwa wa Usubi bado wilaya 24 tu kati ya wilaya hizo 24 wilaya ya Namtumbo inashika nafasi ya tatu kuwa na maambukizi makubwa ya ugonjwa wa usubi.

Baada ya wilaya ya Namtumbo kushika nafasi ya tatu kati ya wilaya 24 ambazo zina hali mbaya ya maambukizi ya ugonjwa wa usubi sasa wilaya hiyo imejipanga kuhakikisha inatokomeza ugonjwa huo huku sababu potofu ya hofu ya kupoteza nguvu za kiume kwa wanaume ikiwa sababu ya kushindwa kutumia dawa za usubi.

Kama ulivyosikia kutoka kwa wataalumu kutoka wizara ya afya wanasema wilaya yetu inashika nafasi ya tatu katika maambukizi ya ugonjwa wa usubi kwahiyo bado tuko kwenye hatari wananchi wanahitaji elimu zaidi ya ugonjwa huo tunapozunguka kutoa dawa tunakutana na changamoto kutoka kwa wanaume kuwa dawa hizi zinaharibu nguvu za kiume.

Nao baadhi ya wanaume wa wilaya ya Namtumbo wamesema wamekunywa dawa hiyo ya kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa usubi na wameona haina madhara yeyote yale hivyo wamewaomba na wananchi wengine watumie dawa hizo.

Nimekunywa dawa hizi za USUBI nimeona hazina madhara yeyote yale nawaomba na wananchi wengine kuzitumia dawa hizi bila hofu yeyote ile.