Dkt Willibrod Slaa
Akizungumza nje ya Mahakama Wakili Philip Mwakilima anayewatetea Wakili Boniface Mwabukusi na Mdude Nyagali amesema mawakili hao wameshaanza kuwasili Jijini Mbeya kwa ajili ya kesi hiyo.
Hata hivyo watuhumiwa hao wanaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Mbeya ikiwa ni siku ya nne bila kufikishwa mahakamani kwa kesi ya uhaini wanayotuhumiwa nayo.
Mwakilima amesema kwa mujibu wa sheria watuhumiwa walipaswa kufikishwa mahakamani leo lakini hawajafikishwa na wanakusudia kufungua kesi kwa lengo la kuiomba Mahakama imlazinishe Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuwafikisha mahakamani au kuwaachilia endapo watabaki wakiwashikilia.