Tuesday , 15th Aug , 2023

Waandishi wa habari takribani wanne na wananchi wapatao wawili wametajwa kuvamiwa na kujeruhiwa na baadhi ya vijana zaidi ya 100 wa jamii ya kimaasai wilayani Ngorongoro, wakati wakifanya mahojiano na wananchi kufuatia zoezi la uhamaji wa hiari katika eneo hilo.

Waandishi waliojeruhiwa

Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro Raymond Mangwala, amethibitisha tukio la waandishi hao kuvamiwa.

Waandishi waliojeruhiwa ni pamoja na Ferdinand Shayo wa ITV, Denis Msacky (mwandishi wa kujitegemea), Habib Mchange (Jamvi la Habari), mkazi mwingine wa Ngorongoro, Lengai Ngoishie. Inaelezwa kuwa vijana hao walikuwa wamebeba mapanga, mikuki, sime na mishale.

Mpaka tunavyotoa taarifa hii Jeshi la Polisi lilikuwa njiani kuelekea eneo la tukio huku sababu kubwa ikitajwa kuwa Wamaasai hao walichukizwa na kitendo cha waandishi hao kuwahoji kuhusu hatma yao ya kuendelea kukaa katika eneo hilo.