Wednesday , 9th Aug , 2023

Timu ya Wanawake ya Yanga Princess imeanza rasmi kambi yake ya Maandalizi Leo Agosti 9-2023 Jijini Dar es Salaam Kwa ajili ya msimu mpya wa ligi kuu ya Wanawake Tanzania Bara 2023-24 inayotaraji kuanza mwezi Disemba 2023.

Akizungumza na EATV, Meneja wa Yanga Princess Mata Gwasa amesema maandalizi yameanza vyema huku Wachezaji wote wameripoti wakiwa na Afya njema na hakuna majeruhi yoyote mpaka sasa.

"Tumefanya Usajili wa kutosha kwa kuingiza wachezaji wengi wenyewe uzoefu na wenyewe vipaji hivyo timu zingine zitarajie ushindani mkubwa kutoka kwetu" amesema Meneja Gwasa.

Kwa upande mwingine Meneja Gwasa amepongeza ukuaji wa soka la wanawake hapa nchini na kusisitiza soka la Wanawake litaleta mafanikio makubwa sana.

"Kwasasa tumepiga hatua katika soka la wanawake na mafaniko ambayo tunayapata katika Ligi yetu ndiyo yanapelekea tunakuwa na timu za Taifa za wanawake zenye wachezaji wenyewe vipaji ambao wanapambana na kutuletea makombe nchinia" amesema Meneja Gwasa

Yanga Princess haijawahi kushinda ubingwa wa ligi kuu ya Wanawake Tanzania Bara huku Msimu uliomalizika 2022-23 walishika nafasi ya 4 nyuma ya bingwa JKT Queens, Simba Queens na Fountain Gate Princess.