Monday , 23rd Feb , 2015

Wakati zoezi la uandikishaji wa wapiga kura katika daftari la kudumu la wapiga kura likianza rasmi leo mkoani Njombe, wasanii wa muziki hapa Tanzania wameungana na kampeni ya EATV ya ZamuYako2015.

Mzee Zahir Zorro

kampeni hiyo ina lengo la kuwataka vijana kujitokeza kwa wingi na kutumia nafasi hii muhimu ili kuweza kufanya maamuzi katika mambo yanayolikabilia taifa ikiwemo uchaguzi mkuu mwaka huu.

eNewz tumezungumza na mkongwe katika gemu ya muziki, Mzee Zahir Zorro na vilevile staa wa muziki wa Bongofleva Kala Jeremiah ambao wamekuwa na ujumbe huu kwa vijana kuhusiana na kujiandikisha kupiga kura.