Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Jenista Mhagama, akikagua miradi
Ameyasema hayo mapema leo 3 August 2023, alipokuwa katika ziara ya kikazi ya kukagua ujenzi wa Jengo la Mpigachapa Mkuu wa Serikali; Jengo la Kituo cha Taifa cha Usimamizi na Uratibu wa Maafa, Jengo la Wizara Mipango na Uwekezaji, na jengo la Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu).
Waziri Mhagama amesema kuwa, ujenzi wa miradi hiyo mikubwa ya kimkakati inayoendelea umewezesha vijana wengi kupata ajira katika maeneo hayo, na kujiongezea pato binafsi sambamba na kuchangia ukuajia wa uchumi kutokana na manunuzi ya bidhaa zinazotumika katika mradi hiyo kufanyika katika viwanda vilivyopo nchini.
"Sisi tumejipanga kwa matumizi ya ndani na nje pia, nimefarijika kuona ujenzi kwa awamu, hii ya kwanza umefikia hatua kubwa, na ujenzi wa Ofisi umeanza na unaenda kwa kasi." Alisisitiza Waziri Mhagama.
Alipokuwa katika kituo cha Taifa cha Uratibu na Usimamizi wa Maafa Mhe. Mhagama alisema, ujenzi wa awamu ya kwanza wa kituo hicho pia umekamilika kwa asilimia 94 na kufafanua kuwa maghala mawili makubwa na Ofisi za Watumishi zimeshakamilika.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi Hiyo Bw. Anderson Mutatembwa, alisema Ofisi hiyo itasimamia kikamilifu maelekezo yote yaliyotolewa na Waziri Mhagama, ikiwa ni pamoja na kuzifanyia kazi chagamoto zilizojitokeza na kuhakikisha zinatatuliwa kwa wakati.
Awali akizungumza katika ziara hiyo, Mwakilishi na Msimamizi Mkuu wa miradi ya Ujenzi kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi Mhandisi Anania Saudeni, Alikiri kuyapokea maagizo ya Mhe. Waziri Mhagama na kuyatekeleza kwa wakati, kimkataba na kukamilika katika ubora kulingana na maelekezo na kuhakikisha kazi zinafanyika usiku na Mchana na kuongeza nguvu kazi ya kutosha na usimamizi madhubuti.