Friday , 28th Jul , 2023

Afisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Arusha Richard Walalaze anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 35-40 amekutwa amefariki dunia baada ya kujirusha ghorofani usiku wa kuamkia leo Julai 28, 2023, katika moja ya Hoteli za Jijini Tanga.

Hoteli aliyojirusha

Taarifa za awali zinaeleza kuwa Afisa huyo amejirusha kutoka ghorofa ya pili ya hoteli hiyo ambako alikuwa amepanga chumba tangu Julai 16.

Afisa hiyo alikuwa miongoni mwa watumishi wa TRA waliokuwa jijini Tanga kwa kazi maalumu ya kuandaa taarifa ya mamlaka hiyo ya mwaka.