
Putin pia ameuambia mkutano wa kilele wa Urusi na Afrika kwamba Urusi inaongeza usambazaji wa chakula kwa Afrika, ikiwa ni pamoja na usafirishaji wa nafaka bila malipo ambayo alitangaza siku moja kabla, na ina nia ya kuendeleza ushirikiano wa kijeshi na bara hilo
Viongozi wa Afrika waliwasilisha mpango wao wa amani mwezi uliopita kwa Putin na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy lakini umeshindwa kupata maelewano na pande zote mbili.