
Kikundi kidogo cha wachomaji moto kilikuwa kimejitenga na onyesho kubwa la kuwaunga mkono viongozi wa mapinduzi nje ya bunge siku ya Alhamisi.
Polisi walirusha vitoa machozi kuwatawanya waliokuwa wamekwenda katika makao makuu ya chama cha PNDS Tarraya, ambako watu pia walikuwa wakipiga mawe na kuchoma magari.
Wizara ya mambo ya nchi hiyo ilitoa taarifa kuwa Maandamano ya hadhara kwa nia yoyote kwa vyovyote vile yanasalia kuwa marufuku hadi itakapo tolewa taarifa nyingineSerikali itahakikisha kwamba sheria inatekelezwa
Ameongeza kuwa Vitendo ambavyo vitafanywa na watu wasio na sheria, vinajumuisha vitendo vya uharibifu na uovu na havitavumiliwa huku wizara hiyo imevitaka vyombo vya usalama kulinda raia na mali zao