Thursday , 27th Jul , 2023

Madereva wa daladala katika kituo cha Mbezi Luis kwenda Mbezi Msakuzi leo waligoma kwa takribani saa saba kusafirisha abiria kwa kile kilichoelezwa kwamba ni muingiliano wa kikazi baina yao na bajaji zinazopaki ndani ya kituo hicho.

Wakizungumza na #EastAfricaTV madereva wa Hiace wamedai kwamba bajaji zimekuwa zinaenda mpaka kwenye gari zao na kuwachukua abiria na kuwapeleka kwenye bajaji kwa kuwatoza shilingi 1000 wakati wao wanatoza nauli ya shilingi 600.

"Bajaji hazifuati utaratibu wa kuchukua abiria ndani ya kituo hiki Kwa kutufanyia vurugu na kuchukua abiria wetu,'' amesema Godfrey John na Hussein Ali ambao ni madereva wa Hiace 

Baada ya mazungumzo kati ya bajaji, polisi na madereva wa hiace madereva bajaji walikubali kupisha kwenye hilo eneo walau ingawa wamedai kutoridhika kusogezwa kwenye kituo

Nao madereva wa bajaji wanaodaiwa kwenda kwenye hiace za Mbezi Msakuzi na kuchukua abiria wamesema kutokea kwa sintofahamu hiyo kumesababisha na madereva wa hiace kutaka waondolewe ndani ya kituo wakati wao waliwekwa kwa kuzingatia taratibu